Wednesday, February 17, 2016

NIFUNZE LYRICS BY JANET OTIENO

Verse1
Funzo la upendo wako ,
hakuna Yule anayeweza kunifunza,
Funzo la upendo wako ,oh oh
Funzo la upako wako,
hakuna Yule anayeweza kunifunza,
Funzo la upako wako,oh oh,
Nimesoma vitabuni ,
na walimu kanifunza lakini sielewi,
marafiki wahubiri na wazazi kanifunza na mimi sielewi,
nimefanya utafiti,
nikatumia mapeni na bado sielewi,
roho wako pekee,
anayeweza kunifunza na mimi nielewe,
oh nataka nikujue,
nijue sauti yako,
na yale yote unapenda ah,
nataka nikujue na niguse uso wako,
na nione ukitenda ah,

(refrain)
nifunze ,nifunze ,
niweze kusema na kutenda,
nitakayofanya  utabasamu,
nifunze ,nifunze ,
niwezeshe kukupenda ,
nataka nione ukitabasamu,x2
verse 2
Afrika mashariki,magharibi ,
kusini kaskazini kila mtu,
ata uchina ujerumani na urusi,
marekani na dunia nzima tukujue,
({ni ombi letu baba x3}
tukujue)x2

(refrain)x2

Ti ti ti
Ti ti ti ti ti ti x2

(refrain)x3

MAVUNO LYRICS BY MIREILLE BASIRWA AND CHRISTINA SHUSHO


Ingawa mtu aenda zake ,akilia,
amechukuapo mbengu,za kupanda,
hakika atarudi ,kwa kelele za furaha,


apandaye haba atavuna haba,
apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu,
jipandie katika haki,
utavuna kwa fadhili,

umetumika kwa machozi,
umepanda mbengu kwa kulia,
husichoke ndugu,
bwana yesu yuko nawe,
jipe moyo wo wo wo ,
asubuhi imefika,

( chorus )
huu ni mwaka wa mavunox4

(shusho)
mwenye kuangalia upepo ,atapanda,
naye atazamaye mawingu,atavuna,
jipe moyo mpendwa,
asubuhi imefika ,msidanganyike,
mungu wetu hadhihakiwi ,
chochote apandaye mtu,atavuna,
ukipanda dhuluma,utavuna uovu,
ukipanda mema utavuna mema,
chochote upandacho,ndicho utavuna,

umetumika kwa matusi ,
umepanda mbengu kwa kulia,
husichoke mpendwa,
utavuna kwa wakati wako,

( chorus )

Saturday, February 6, 2016

ITAKUWA SAWA LYRICS BY BAHATI

verse 1
Nilipotenganishwa tu na mama,
niliingia kwa mtaa kutafuta butter,
masela walinata,
huku na kule tumaini la kupata,
nisije na uchungu,
mito mikubwa milima nilivuka,
natumaini tu kwa mungu,
awape nguvu nyumbani niliowacha,

nikaamua niende mbali,
ii mbali na nyumbani,
nikamua niende mbali,
ili kusaka ugali,
nikaamua niende mbali,
nikaamua niende mbali,
mbali na,

(chorus)

itakuwa sawa
kwa hivi waeleze nyanya na babu
itakuwa sawa,
shangazi mwambie hasife moyo,
itakuwa sawa x2

verse 2
na hivi msichoke ,
kukopa dukani paendapo pangumu
hivi mniombee,
maisha mjini bado ni sugu x2

naelewa na uchungu uliowabana,
naelewa si rahisi kupambana ,
naelewa na majozi yamewakumba,
mama baba,
naelewa na uchungu uliowabana,
si rahisi kupambana ,
naamini tukimwamini rabana,
yote

(chorus )

verse 3
napita mengi na si utani,
wambie eh
sijadanganywa na burundani ,
wambie eh
x2

(Chorus)

mweleze na nyanya,
mweleze mjomba,,(itakuwa sawa)
mweleze masela 
musyoki wa benga,(itakuwa sawa)
mweleze susana,,(itakuwa sawa)

na hivi msichoke.