Tuesday, September 19, 2017

FUNGUO LYRICS BY FLORENCE ANDENYI FT.MARTHA MWAIPAJA


yesu nipe funguo,baba nipe funguo,
yesu nipe funguo kwa huduma yangu,
yesu nipe funguo,baba nipe funguo,
naomba unipe funguo kwa maisha yangu
nipe funguo baba ,nipe funguo yahweh,
oh naomba funguo,

naamka asubuhi naenda tafuta riziki,
naondoka naenda tafuta riziki,
ili niwalishe ndugu na jamaa zangu,
nikifika milango imefungwa,
nikifika milango imefungwa,
oh naomba funguo,yesu
nipe funguo,

chorus
nipe funguo,
naomba nipe funguo kwa maisha yangu

nimetoka mbali mimi,
nimejitahidi sana,mimi
nimejitahidi sanakushinda haya mangumu
nimekimbia sana mimi,
nimetembea sana mimi baba,
imefika wakati sasa nimechoka,
miguu yangu imelegea nimekosa nguvu,
maana nilifikiri hapa kutakuwa mwisho wangu,
kumbe bado safari ninayo,
kumbe bado natakiwa kuendelea,
nami  baba nipe funguo,
ili nifike pale ,nipe funguo,
 milango ya pale yote imefungwa,
nipe funguo,baba

chorus
nipe funguo,
naomba nipe funguo kwa maisha yangu

hela ya kodi nimelemewa nyumba nimefungiwa,
marafiki wananicheka,bwanaa,
nimekosa tumaini,nimekosa msaada,
msaada wangu watoka wapi eh baba,
kupitia kwa moto nimepitia mie,
kama ni gharama,nimelipa mie,
kupitia kwa moto nimepitia mie,
oh kama ni gharama nimelipa mie,
oh yesu nipe funguo,baba nipe funguo,

chorus
nipe funguo,
naomba nipe funguo kwa maisha yangu

mmh,wewe ni tabibu ganga jeraha zangu,
moyo unalia mimi nakusubiri,
hatua zangu ni fupi siwezi kwenda mwenyewe,
baba siwezi bila wewe oh,
baba siwezi bila wewe oh,
ukinishika mkono wangu,
nitaenda mwenyewe,
ukinishika mkono wako nitaenda vizuri


chorus
nipe funguo,
naomba nipe funguo kwa maisha yangu



2 comments:

Unknown said...

Please give English translation

thanks

Unknown said...

I'm deeply inspired by this and i vow to serve my Lord in True Spirit.i will do a cover for this one day