Pages

Monday, October 19, 2015

SOMA MWANANGU LYRICS BY BONY MWAITEGE




Verse1
Mshike sana elimu usimwache aende zake,
ni maneno ya mungu kutoka kwenye vitabu vitakatifu ,
mimi enzi zangu maneno hayo si kuyajua,
 nilifanya mchezo sikuweka uzito kwenye elimu ,
hivyo, nilishindwa kusoma,
 ndio maana namuomba mungu mtoto wangu usome ,
hivyo mimi baba yako nilishindwa kusoma ,
ndio maana namuomba mungu mtoto wangu usome,
 soma

(refrain)
Baba yako anapenda ,mwanangu usome,
mama yako anapenda ,mwanangu usome

Verse2
Namuomba mungu akusaidie sana mwanangu usome (Refrain)
Namuomba mungu akupiganie wewe mwanangu usome (Refrain)



Verse3
Husifanye mchezo ukiwa darasani mwanangu,
mimi na mama yako tunapenda sana usome ,
ukifanya mchezo maisha yetu mwenyewe unayajua,
ukifanya mchezo tutakuwa wageni wa nani,
Soma ,soma mwanangu,
soma we,soma mwanangu pengine,
 utakuja kutuokoa we,baadaye
(Refrain)

Verse4
Mimi baba yako sikubahatika kusoma ,
soma mwana(Refrain)

usome wewe,
 pengine unaweza okoa familia yetu(Refrain)

Kazi ya ulinzi ni ngumu nakulilia we usoma,
 soma we mwanangu(Refrain)

Nabeba kirungu nanga’twa na mbu usiku kucha,
 kwa ajili yako mwanangu,soma we(Refrain)

Maisha bila kusoma ni magumu mwanangu(Refrain)
Mimi na mama yako hatuchoki kukuombea we(Refrain)

Mungu akusaidie,
 usome mwanangu,usome(Refrain)

Nimebeba zege,
 pesa zote nimepeleka shuleni(Refrain)

Robo tatu ya mshahara wangu wote ,
nimepeleka shuleni (Refrain)

Tumeuza ng’ombe pesa zote tumepeleka shuleni(Refrain)
Tunamuomba mungu wa mbinguni afanye njia(Refrain)
Mama yako kauza chapati pesa zote tumepeleka shuleni(Refrain)
Verse5
Mambo niliyoyafanya nikiwa shule sitaki ata kuyakumbuka ,
Moyo wangu unauma kila nikikumbuka,
 maisha magumu ninayoishi,
 uzembe wangu umechangia,
nilifanya mchezo nikiwa shule mwanangu,
niliona sifa ,daftari yangu kujisahishia ,
Leo hii najuta, natamani kusoma ,
,niliona sifa, kutoroka shule kupitia dirishani,
 leo hii najuta, natamani kusoma ,
napendwa na wazungu,
 lakini lugha inanikosa,
 leo hii najuta natamani kusoma,
 nikimwona mzungu kwa mbali nabadilisha njia,
 naogopa hasije akinisemesha how are you,
 na lugha sijui ,soma mwanangu ,soma, soma we
(Refrainx3)
Verse6
Jitume kusoma na sisi tunajituma kukuombea (Refrain)
Ukisoma kwa bidii ,mungu atafanya njia mwanangu(Refrain)
Mungu amesisitiza tusiachae elimu iende zake(Refrain)
Ukijituma mungu anakukumbuka ,
mamayako pia anapenda mwanangu usome

No comments:

Post a Comment

Write a correction.