Pages

Friday, November 20, 2015

MAMA MKWE LYRICS BY ROSE MUHANDO

Verse1
Mbona nasikia kelele, kutoka  nyumba ya pili,
Nasikia mayowe  kutoka mtaa wa pili,
Sauti ya ukali sana ,ikisema maneno ya ajabu,
Mara mwanamke gani, mara ana sura baya,
Mara miguu kushoto mtupu,
 mara ana kicheko kibovu,

verse2
Katika shumaka ya  dirisha langu nalichungulia,
 nione kuliko nini,inaendelea nini,
niliyoyaona jameni we ni vigumu kusimulia,
kumbe mama mkwe ameleta balaaa eeh
jamani mama mkwe anatia aibu eeh
nasema mama mkwe amezua kizaazaa,

verse3
yanatutisha yanatutisha ,yanatuogopesha jamani,x2
tulio katika nje ya ndoa twaogopa kuingia,
maneno ya mama mkwe ni makali sana eeh,
mara ana sura baya ,
mara ana shape baya,mwanamke ana sura baya,
mwanamke ana shape baya,
hajui kuvaa viatu,
 mama mkwe ni mshamba mkubwa,aah
mama mkwe ana tabia baya ,
wewe mama mkwe ,unatia aibu

verse4
poleni wanandoa ( poleni)x2
nilioyasikia pia nataka kuyasimulia,
niliyoyaona kwa macho yangu ,lazima niwambie,
niliyoyasikia ya mama mkwe magumu kusimulia,
niliyoona kwa macho yangu we, lazima niwambie,
mama mkwe kizaazaa ,mama mkwe kizunguzungu,
mama mkwe kiherehere ,anatia aibu,

verse5
nataka nikuulize mama mkwe nisikilize,
tangu  ulipokuja mjini ,
kwenye ndoa ya mwanao,
hujageuza kisogo mama
kurudi kijijini kwa mumeo,
mama unataka nini mama mkwe,
mke mwana akinunuliwa kitenge mama mkwe unadai,
akinunuliwe kiatu,ata wewe unadai,
akitolewa out, mama mkwe unanuna,
akicheka na mumewe ,eti unatema mate,
mama unataka nini mama mkwe,
nauliza unataka nini ,kwenye ndoa ya mwanao,

verse6
upende husipende eeh,
mama mkwe lazima nikwambie nikwambie aah aah
imeandikwa ya kwamba atawaacha baba na mama,
ataambatana na mkewe watakua mwili mmoja,
na wewe umetoka wapi mama mkwe,
nakuuliza umetoka wapi mama mkwe,
eti wewe umetoka wapi mama mkwe,
mbona mama kizaazaa,
 mama mkwe kizunguzungu,
mbona mama tafrani,
mama mkwe kiherehere,
mama mkwe kizaazaa unatia aibu wee,

verse7
ulipoona imeshidikana kuachanisha ndoa ya mwanao,
ukatafuta mbinu mpya ili ung’oe ndoa ya mwanao,
ukaenda kwa waganga , ndoa ya mwanao ivunjike,
mara akasema hivi,naye mwisho umefika ,
hivi mama unataka nini mama mkwe ,
mama mbona una mateso mama mkwe,
mbona unaitesa sana ndoa ya mwanao,
akaoe nani,akampende nani,x2
ata kama angepaa mbinguni aoe malaika,
ata kama angepanda  mbinguni akaoe malaika,
ulivyo na tabia yako lazima ungemtoa kasoro,
mama mkwe una tabia baya ,mama mkwe eeh,
mama mkwe jirekebishe unatia aibu,

verse8
siku nyingi nimesikia makelele kwa wanandoa ,
lakini chanzo ,ni wewe mama mkwe,
lakini taabu ni wewe mama mkwe,
nasema tafrani,ni wewe mama mkwe,
kuvunjika ndoa za watoto wenu
tatizo ni mama mkwe,
mama jirekebishe mama mkwe,
nasema jirekebishe unatia aibu,
message sent ukidelete ujumbe umefika,

(aibu we )x3
unatia aibu  x6

No comments:

Post a Comment

Write a correction.