Monday, November 30, 2015

POKEA SIFA LYRICS BY FLORENCE ANDENYI




( Refrain)
Pokea sifa x4,
 kwa matendo yote uliyotenda,
 pokea sifa ,
Kwa neema yote dunia nzima amen,
Halleluyah ooh.

Verse1
Nilikuwa nasimuliwa matendo yako,
Nikasimuliwa wema wako ,
Nani kama wewe eeh yesu,
Ooh uliponya vipofu wakaona ,
tena ukafanya visiwi wakasikia,
ona umefanya viwete wakatembea ,
ooh Samaki wawili mikate mitano ,
ulilisha watu elfu tano,
Ooh yesu we,
(refrain)


Verse2
Ooh nikikosa mavazi utanivisha ,
tena nikikosa chakula utanilisha,
nikikumbwa na magonjwa utaniponya,
mponyaji wa roho yangu ni wewe yesu ,
Kimbilio la maisha yangu ni wewe baba ,ooh

Verse3
Kama vile ulituliza bahari yesu we
Kama vile ulituliza mawimbi baba,
Tuliza magonjwa yote leo,
Tuliza na shida zote leo

Kama vile ulituliza mawimbi baba,
Kama vile ulituliza bahari yesu we
Tuliza mawazo yangu leo,
Tuliza kilio change leo

(Refrain)

No comments: