Pages

Monday, October 7, 2024

KAA NAMI LYRICS BY ISRAEL MBONYI


Chorus 
Ikiwa nimepata neema kwako, unikumbuke 
Jicho lako liwe juu yangu nyakati zote 
Wema wako unisindikize Hadi tamati 
Hili ni ombi langu, nakumwagia moyo Ninachoomba kaa nami 
ikiwa nimepata neema  kwako

1. Kutakuwa milima haitaondolewa 
Kutakuwa na mito na sitaweza kuvuka 
Sio kila ombi litajibiwa nipendavyo 
Sio kila wimbo utakaotuliza moyo 

Nimekupata, nina mtetezi 
Unionyeshe njia zako 
Nikujue.

2. Kumbuka hayo mema niwaombeayo wanaonifurahia 
maadui zangu nao, uwape kukujua 
Uwabaliriki kwa utele uwanyeshee mvua 
yamkini watapata kuona 
Wapumue upendo.

Tunaoshiriki hii huduma, 
uwape uamsho 
Uwabaliriki kwa utele , 
Baba wala-hi-sishie. 

3.Kwa maswali na majibu,
umasikini utajiri, usumbufu utulivu 
Ewee Mwokozi kaa nami 

Kwa kupanda kwa kushuka, 
habari za kuvunja moyo 
Kwa uzushi na uongo 
Ewee Mwokozi kaa nami.

No comments:

Post a Comment

Write a correction.