Verse1
(Nabii Elijah, aliwaita manabii wote,
wa mungu baali)x2
Lengo la elija,
ilikuwa ni kumthibitisha
mungu wa kweli ni yupi,
kati ya mungu wa baali, na
mungu wa mbinguni ,
(Elijah )x2, akawambia watu nikaribieni mimi
akachukua mawe kumi na mbili akaanza kujenga madhabau,
akaweka kuni juu yake,
akaweka sadaka juu yake,
akachimba mfereji ,
akawambia watu mwageni maji mapipa manne ,
wakamwaga maji mara ya kwanza ,
wakamwaga maji mara ya pili,
wakamwaga maji mara ya tatu ,
Elijah, akaanza kumuita mungu,
mungu wa mbinguni (we mungu )x2,
( mungu wa mbinguni naijulikane kuwa upo)x2
Moto ukashuka ,ukaramba ile sadaka,
ukaramba zile kuni ,ukaramba na yale mawe,
ukaramba na yale mavuno ,
ukaramba na yale maji ,watu wakasujudu,
wakasema huyu ndiye mungu,
anayepaswa kuabudiwa ,
ndiye mungu ninaye mwimbia mungu wa Elijah,
(Refrain)
oooh mungu
( Mungu ni mungu tu,atabaki kuwa mungu tu)
Ooh mungu baba
Huyu mungu wa mbinguni jamani
Huyu mungu wa elijah
Maishani mwako mama yangu wee
Mahali pote unapotembea
Ata wainuke wamseme vibaya
Ata wamkatae mbele yako
Verse 2
Na wewe ndugu yangu,
unayenisikia, unaye
nitazama,
(unaona nini mbele yako)x2,
pengine unaona majaribu,
haujui utafanya nini,
we mkaribie mungu tu,
pengine unaona magonjwa,
haujui utapona lini we
mkaribie mungu tu,
pengine unaona vita kubwa,
haujui utashinda vipi, we
mkaribie mungu tu,
Pengine unaona watesi ,
haujui utapita vipi, we mkaribie mungu tu,
pengine ni jaribu katika ndoa yako,
haujui utashinda vipi,
we mkaribie mungu tu ,
(hakuna linaloshidikana kwake mungu)x4
Aliyemshindia elijah ,
katikati manabii wa baali atakushindia
Na wewe …..
(Refrain)
Verse 3
Wanadamu wamekusemea maneno,
kwamba hautaweza ,katika
jaribu lako,
wanadamu wamekusemea maneno,
kwamba hautashinda katika
vita yako,
kumbe( njia za mungu, sio
sawa na za mwanadamu )x2
mipango ya mungu ,sio sawa
na ya mwanadamu,
akili ya mungu, sio sawa na
ya mwanadamu
Maneno ya mungu, sio sawa na ya mwanadamu
Mawazo ya mungu, sio sawa na ya
mwanadamu
Kazi ya mungu, sio sawa na ya
mwanadamu
Sauti ya mungu ,sio sawa na ya
mwanadamu
Aliye mshindia elijah ,
katikati ya manabii wa baali
atakushindia na wewe ……
(refrain)
No comments:
Post a Comment
Write a correction.