Pages

Saturday, October 31, 2015

PENINAH AND ANNAH LYRICS BY SOLOMON MUKUBWA


Verse1
Paalikuwa na wanawake wawili,
kwenye biblia,mmoja allitwa annah ,,aah,
na mwingine aliitwa penninah,
Peninnah kajaliwa na watoto ooh
Annah hakujaliwa na mtoto ooh
Ikawa uchochezi kwa annah,
annah akipita penninah anamchukia tu,
watoto wako uliwakulia wapi wewe annah,
Penninah akamsumbua annah,
penninah akamkosesha annah amani,eeh
annah akakaa akiumizwa kwa moyo wake,
Akifikiri sitamgombesha penninah ,
akafikiri sitajibishana na penninah,
kwa maana anayoyaongea ni ukweli,
kusema kweli mimi sina mtoto ,
kusema kweli yeye ana watoto,
ya muhimu nitafanya ,
nitamuendea muumba wangu,
aliyeniumba kama yeye ,
aliyempa watoto kama yeye
(na mimi anikumbuke,kweli)x2
Kama alivyomkumbuka penninah

(Refrain),
Unikummbuke bwana ,
ili jina lako litukuzwe,
unikumbuke bwana madui washangae,
unikumbuke bwana ili nitoe (ushuhudax3),
unipe( ushuhudax3),
unipe ushuhuda wako ,

verse2
Penninah una nini na annah,
penninah annah kakufanyia nini
una tumbo la kwako,
annah naye ana la kwake,
kama wewe utajaliwa mtoto mbele,
ni mungu amekupa,
kila mtu na wakati wake,
wengine wanatembea na ahadi za mungu,
annah kachukua mimba,
kamzaa mtoto wa ahadi,
akaitwa samuel,nabii wa Israeli,
mbona wa kwako penninah
hatuwajui kwa biblia,
annah kabarikiwa na samuel,
penninah funga kinywa,
annah amezaa mtoto,
penninah funga kinywa
utamshtumu kwa lipi tena

(refrain)

Verse3
Kuna wengi wako kama annah, makanisani,
Wanangojea muujiza kutoka kwa mungu ,
husiseme mungu amaechelewa ,
atakubariki tu,
Ya kwako itakuwa kubwa sana,
kama ya annah,utaacha historia duniani,
mama ,na wengine wako makanisani,
wako kama penninah,
kazi yao ni kuleta vurugu kwa ma-annah ,
mungu amepeana vipawa mbalimbali wivu imewatesa,
tulia wewe penninah,
mungu ajua walio wake,
tulia we penninah ,
atashughulikia watu wake mungu uuh,
ukuwacheka leo,wanaenda kuiga historia ,
ukiwaona leo hawafai  ,
kesho utashangaa penninah,
eeeh mungu wa annah yuko

(Refrain)

3 comments:

  1. Hie i have been looking for this song online without trace... can u assist with a link to it... uptowncompsatgmail

    ReplyDelete
  2. Sorry Uptown Computer Centre i do not have an official version i wrote the lyrics from a version i recorded from my radio. I have been looking for an official version on most of the music shops to no avail

    ReplyDelete
  3. I am in the same situation. Kindly if you ever found a link for the song, just share with me through alubef13@gmail.com

    ReplyDelete

Write a correction.