Thursday, August 20, 2015

WAKATI NITAJIKUTA MBINGUNI LYRICS BY ELKANT

Wakati nitajikuta, mbinguni kwa baba,
Nitajua ya ulimwengu nimeshayaacha,
Halleluya nitasifu, kufika mbinguni,
Hossana nitaingia kwa shangwe


[Refrain]
Nitaingia lango lake na sifa moyoni,
Nitaingia kwa shangwe kuu,
Nitasema ni siku njema bwana ameifanya,
Nitafurahi kufika mbinguni X2

Nchi nzuri nchi safi, kwa baba yangu,
Kuna amani kuna furaha, uko ni kusifu,
Tutakaa na mungu wetu, nchi ya amani,
Hossana nitaingia kwa shangwe,


[Sing Refrain twice]

Nitawaona watakatifu, manabii wote
Hata mitume nchi hiyo, nitawaona,
Tutakula mezamoja, nchi ya amani,
Hossana nitaingia kwa shangwe.

[Sing Refrain twice]





2 comments:

Anonymous said...

Amen 🙏

Anonymous said...

HALLELUJAH 🙏🙏🙏