Showing posts with label SOLOMON MUKUBWA. Show all posts
Showing posts with label SOLOMON MUKUBWA. Show all posts

Sunday, April 17, 2016

MUNGU MWENYE NGUVU LYRICS BY SOLOMON MUKUBWA

Verse 1:
Mungu wetu mwenye nguvu, ni Baba wa milele
(Mungu wetu mwenye nguvu, Baba wa milele) – (Refrain 1 )
Mwenye nguvu, Ebeneza wa milele
Wanipa mema, wewe ni mwenye nguvu, Baba wa milele
Nguvu zako zashangaza dunia,
uliumba mbigu pasi kugusa, hewani Baba

Refrain 2:
Neema, fadhili zako, kila asubuhi
Ulizotenda zanifariji moyo niamkapo

Verse 2:
Nikikosewa na maisha, wanipa tumaini la kupata maisha Baba
Japo wanicheka majirani
Wewe upo upande wangu, Uhimidiwe Yahweh

Verse 3:
Wanipa tumaini la maisha Baba yangu duniani
Natembea nawe Baba yangu,
Hujaniacha mimi

(Refrain 2) + (Verse 3)

Verse 4:
Kulala, kuamka ni kwa neema yako
Ndugu yangu Ulimpa mungu nini wewe
kusudi uwe jinsi ulivyo?
Usijivune bure ni neema yake baba.

(Refrain 2)

Refrain 3:
Baba utukuzwe, Baba uinuliwex3

Rafiki yangu, I love you, I love you + Refrain 3
Maneno yafungua watu  + Refrain 3
Sitasahau uliponitoa , Umenitoa mbali + Refrain 3

(Refrain 3)

Translation
Verse 1:
Mungu wetu mwenye nguvu, ni Baba wa milele (Our mighty God, is the everlasting Father)
(Mungu wetu mwenye nguvu, Baba wa milele) – (Refrain 1 )
Mwenye nguvu, Ebeneza wa milele (He has the mighty, everlasting Ebenezer)
Wanipa mema, wewe ni mwenye nguvu, Baba wa milele (You grant me good things, you are mighty everlasting Gather)
Nguvu zako zashangaza dunia,
uliumba mbigu pasi kugusa, hewani Baba (Your might astonishes the world, you created the world by the word of your mouth )

Refrain 2:
Neema, fadhili zako, kila asubuhi ( Your goodness and mercies, every morning)
Ulizotenda zanifariji moyo niamkapo (And your works comfort me when I awake)

Verse 2:
Nikikosewa na maisha, wanipa tumaini la kupata maisha Baba (When I am slighted in life, you give me hope in life)
Japo wanicheka majirani ( Though my neighbors laugh at me)
Wewe upo upande wangu, Uhimidiwe Yahweh ((You are in my side, Be praised Yahweh))

Verse 3:
Wanipa tumaini la maisha Baba yangu duniani ( You give me hope in life My Father)
Natembea nawe Baba yangu, ( I walk with you my Father)
Hujaniacha mimi ( You haven’t abandoned me)

(Refrain 2) + (Verse 3)

Verse 4:
Kulala, kuamka ni kwa neema yako (When I sleep, and wake, it is by your grace )
Ndugu yangu Ulimpa mungu nini wewe ( My brother, what did you give God)
kusudi uwe jinsi ulivyo? (For you to be the way you are?)
Usijivune bure ni neema yake baba. ( Do not boast, it  is by grace of God)

(Refrain 2)

Refrain 3:
Baba utukuzwe, Baba uinuliwe (Father be praised, Father be lifed up ) x3

Rafiki yangu, I love you, I love you Father yo ( My friend I love you, Father) + Refrain 3
Maneno yafungua watu ( Your words releases prisoners) + Refrain 3
Sitasahau uliponitoa , Umenitoa mbali ( I will not forget the distance you’ve brought me) + Refrain 3

(Refrain 3)

Saturday, October 31, 2015

PENINAH AND ANNAH LYRICS BY SOLOMON MUKUBWA


Verse1
Paalikuwa na wanawake wawili,
kwenye biblia,mmoja allitwa annah ,,aah,
na mwingine aliitwa penninah,
Peninnah kajaliwa na watoto ooh
Annah hakujaliwa na mtoto ooh
Ikawa uchochezi kwa annah,
annah akipita penninah anamchukia tu,
watoto wako uliwakulia wapi wewe annah,
Penninah akamsumbua annah,
penninah akamkosesha annah amani,eeh
annah akakaa akiumizwa kwa moyo wake,
Akifikiri sitamgombesha penninah ,
akafikiri sitajibishana na penninah,
kwa maana anayoyaongea ni ukweli,
kusema kweli mimi sina mtoto ,
kusema kweli yeye ana watoto,
ya muhimu nitafanya ,
nitamuendea muumba wangu,
aliyeniumba kama yeye ,
aliyempa watoto kama yeye
(na mimi anikumbuke,kweli)x2
Kama alivyomkumbuka penninah

(Refrain),
Unikummbuke bwana ,
ili jina lako litukuzwe,
unikumbuke bwana madui washangae,
unikumbuke bwana ili nitoe (ushuhudax3),
unipe( ushuhudax3),
unipe ushuhuda wako ,

verse2
Penninah una nini na annah,
penninah annah kakufanyia nini
una tumbo la kwako,
annah naye ana la kwake,
kama wewe utajaliwa mtoto mbele,
ni mungu amekupa,
kila mtu na wakati wake,
wengine wanatembea na ahadi za mungu,
annah kachukua mimba,
kamzaa mtoto wa ahadi,
akaitwa samuel,nabii wa Israeli,
mbona wa kwako penninah
hatuwajui kwa biblia,
annah kabarikiwa na samuel,
penninah funga kinywa,
annah amezaa mtoto,
penninah funga kinywa
utamshtumu kwa lipi tena

(refrain)

Verse3
Kuna wengi wako kama annah, makanisani,
Wanangojea muujiza kutoka kwa mungu ,
husiseme mungu amaechelewa ,
atakubariki tu,
Ya kwako itakuwa kubwa sana,
kama ya annah,utaacha historia duniani,
mama ,na wengine wako makanisani,
wako kama penninah,
kazi yao ni kuleta vurugu kwa ma-annah ,
mungu amepeana vipawa mbalimbali wivu imewatesa,
tulia wewe penninah,
mungu ajua walio wake,
tulia we penninah ,
atashughulikia watu wake mungu uuh,
ukuwacheka leo,wanaenda kuiga historia ,
ukiwaona leo hawafai  ,
kesho utashangaa penninah,
eeeh mungu wa annah yuko

(Refrain)

Friday, October 9, 2015

NIMEWASAMEHE LYRICS BY SOLOMON MUKUBWA




Verse1
 Mmmh …Ooh ,oooh,
Nilipokuwa mtoto,
nilizaliwa kama wewe,
 viungo vyote vya mwili ,
vilikuwa kama wewe,
 ghafla dunia ,mambo yakageuka,
nikajikuta kiugo kimoja, kimeniondokea,
 mimi nikajua kuwa, mwisho wa mambo yote imefika,
 wala sifai, nikaona dunia imenitupa ,
nikaona dunia imenidharau,
nikajidharau mwenyewe nikajua sasa mimi,
 sifai tena, niliwanung’unikia,
 wote waliohusika, kwa haya mambo,
 roho ya kisasi ikaja juu yangu,
nikajua sasa na mimi ,nitalipa kisasi,
 kumbe kunaye mungu ,mungu wa visasi
Akaniambia, Solomon nina mpango na wewe ,
lazima piga hatua ,uwasamehe kwanza,
 ooh nikabishana na mungu ,
Wote walionitendea mabaya ,
mimi siwezi wasamehe,
Moyoni mwangu ,bwana kaniambia ,
wataka nitumike na wewe,
 nina  ahadi zuri na wewe,
kuhusu dunia hii ukitaka nitumike na wewe ,
uwaachilie wote,uliowaweka moyoni mwako ,
nikapiga hatua nikawasamehe,
 wote walionikosea
Bwana katumika na mimi ooh

(Refrain)
Nimewasamehe wote)x2 ,
nimewasamehe kutoka moyoni mwangu,
(nimewachilia wote)x2,
nimewachilia kutoka moyoni mwangu x2
verse2
Tumekunywa damu ,damu ya yesu,
tumekula na mwili wa yesu ooh,
mwili wa yesu ni msamaha,
 aah tujikane wenyewe,
Mara nyingi tumeonekana wajinga duniani,
dunia imeshindwa kutuelewa wakristo, eeh
Umetendewa mabaya ,lakini neno linasema,
 kubali nenda ukaombe msamaha,
ki kawaida ya dunia,
 ukinitendea mabaya lazima ooh ieleweke,
lakini kwetu sisi wakristo ,
ukinitendea mabaya ,mimi lazima nikusamehe,
 sababu nisipokusamehe
Baba yetu wa mbinguni ,
na yeye hawezi nisamehe,
 haijalishi unapitia nini,
kama wewe umeokoka,
huwasamehe waliokukosea ooh eeh
Husifanye moyo walo jela,
 kuwafungia watu, amua leo uwaondoe,
 ili mungu wetu akubariki ,
samehe jirani yako,
 mungu na yeye atakusamehe 
(Refrain)


Verse3
Ni vigumu jamani mara nyingi ,
kuna mambo ambayo tunapitia ,
mwenzako mwanadamu anakupitisha kwa mambo mazito,
 lakini ,unapaswa hufanyeje ,
ashurukuriwe mungu sababu neno la mungu linasema tusamehe tu,
na tumevaa mwili wa yesu,
tumekunywa damu ya yesu,
kumbuka msalabani,
 yesu aliwaponya watu,
viwete wakatembea mabubu wakaongea,
akawalisha watu, zaidi ya elfu tano,
lakini wale watu ndio walimuweka msalabani,
 mwisho msalabani ikasema baba wasamehe,
 huwasamehe, ,kumbuka stephano,
 stephano  alikuwa anapigwa mawe ,
alipokuwa anapigwa mawe,bibilia inasema ,
stephano kaambia baba huwasamehe,
maana hawajui wanalolitenda bibilia inasema
 stephano akaona mbingu zinafunguka ,
kwenye msamaha kuna nguvu,
 kwenye msamaha kuna uwezo,
stephano hakujali tena mawe wanayomtupia ,wanayomchapa
Lakini stephano alikuwa ameona mbingu zimefunguka,
 na tayari anakwenda kupokelewa,
Msamahe jirani yako ,
kusudi uone mkona wa mungu,
Husimfungie kwenye moyo wako ,
utakuwa umujizuilia baraka yako,
msamehe muachilie tu,
Maana tumevaa mwili wa yesu,
 na tumekunywa damu ya yesu,
ooh yesu tusaidie kuwasamehe waliotukosea



verse 4
Pengine una watu,
 ambao umefungia moyoni wala hutaki kuwasamehe,
 nakwambia leo, fungua moyo wako,
ili mungu wa mbinguni akusamehae,
husijiwekelee vikwazo ,
maisha ni mafupi yesu yu karibu kuja,
huwasamehe wote waliokukosea,
Ili uone mbingu ooh, hatujui ya kesho ,
ya kesho ni ya mungu ,
fungua moyo wako leo ,yule uliye mkopa hela ,
kashindwa kurudisha, sasa leo amekutusi ,
na yeye umsamehe,
 uwe safi mbele ya mungu yesu yu karibu kuja
(refrain)