Tuesday, April 7, 2015

KWETU PAZURI LYRICS BY AMBASSADORS OF CHRIST CHOIR RWANDA


Ninayo hamu kurudi nyumbani
Nyumbani kwetu ambapo hatutatengana
hapo nyumbani kwetu hakuna makaburi
Wala hakuna vyandarua maana hakuna malaria
Kwetu pazuri ni pazuri nakuambia
Najua nawe ndugu yangu unayo hamu kufika huko


kwetu pazuri nimeshapakumbuka
Ninayo hamu kuishi na mwokozi wangu
Kwa amani na furaha tena ya ajabu
Sipati picha kwa watakaofika kwetu mbinguni*2


Hii dunia imejaa shida kama hujui nenda hospital kaone
Lakini kwetu hakuna fani ya tabibu
Watakatifu watachuma majani ya mti wa uzima wawe na afya
Hawataugua magonjwa tabu tutaziacha zote hapa duniani

Mpendwa njoo, turudi nyumbani
Asubuhi yaja tuyakimbie ya dunia
Atayekosa hapo kweli ni hasara
Aya matatizo ni mitego ya shetani
Hili tushindwe kufika nyumbani kwetu pazuri
Lakini kwa jina jina la Yesu tumemshinda tunaenda

No comments: