Verse1
Mbona nasikia kelele, kutoka nyumba ya pili,
Nasikia mayowe kutoka mtaa wa pili,
Sauti ya ukali sana ,ikisema
maneno ya ajabu,
Mara mwanamke gani, mara ana sura
baya,
Mara miguu kushoto mtupu,
mara ana kicheko kibovu,
verse2
Katika shumaka ya dirisha langu nalichungulia,
nione kuliko nini,inaendelea nini,
niliyoyaona jameni we ni vigumu
kusimulia,
kumbe mama mkwe ameleta balaaa
eeh
jamani mama mkwe anatia aibu eeh
nasema mama mkwe amezua kizaazaa,
verse3
yanatutisha yanatutisha ,yanatuogopesha
jamani,x2
tulio katika nje ya ndoa twaogopa
kuingia,
maneno ya mama mkwe ni makali
sana eeh,
mara ana sura baya ,
mara ana shape baya,mwanamke ana
sura baya,
mwanamke ana shape baya,
hajui kuvaa viatu,
mama mkwe ni mshamba mkubwa,aah
mama mkwe ana tabia baya ,
wewe mama mkwe ,unatia aibu
verse4
poleni wanandoa ( poleni)x2
nilioyasikia pia nataka
kuyasimulia,
niliyoyaona kwa macho yangu
,lazima niwambie,
niliyoyasikia ya mama mkwe magumu
kusimulia,
niliyoona kwa macho yangu we,
lazima niwambie,
mama mkwe kizaazaa ,mama mkwe
kizunguzungu,
mama mkwe kiherehere ,anatia
aibu,
verse5
nataka nikuulize mama mkwe
nisikilize,
tangu ulipokuja mjini ,
kwenye ndoa ya mwanao,
hujageuza kisogo mama
kurudi kijijini kwa mumeo,
mama unataka nini mama mkwe,
mke mwana akinunuliwa kitenge
mama mkwe unadai,
akinunuliwe kiatu,ata wewe
unadai,
akitolewa out, mama mkwe unanuna,
akicheka na mumewe ,eti unatema
mate,
mama unataka nini mama mkwe,
nauliza unataka nini ,kwenye ndoa
ya mwanao,
verse6
upende husipende eeh,
mama mkwe lazima nikwambie
nikwambie aah aah
imeandikwa ya kwamba atawaacha
baba na mama,
ataambatana na mkewe watakua
mwili mmoja,
na wewe umetoka wapi mama mkwe,
nakuuliza umetoka wapi mama mkwe,
eti wewe umetoka wapi mama mkwe,
mbona mama kizaazaa,
mama mkwe kizunguzungu,
mbona mama tafrani,
mama mkwe kiherehere,
mama mkwe kizaazaa unatia aibu
wee,
verse7
ulipoona imeshidikana kuachanisha
ndoa ya mwanao,
ukatafuta mbinu mpya ili ung’oe
ndoa ya mwanao,
ukaenda kwa waganga , ndoa ya
mwanao ivunjike,
mara akasema hivi,naye mwisho
umefika ,
hivi mama unataka nini mama mkwe
,
mama mbona una mateso mama mkwe,
mbona unaitesa sana ndoa ya
mwanao,
akaoe nani,akampende nani,x2
ata kama angepaa mbinguni aoe
malaika,
ata kama angepanda mbinguni akaoe malaika,
ulivyo na tabia yako lazima
ungemtoa kasoro,
mama mkwe una tabia baya ,mama
mkwe eeh,
mama mkwe jirekebishe unatia
aibu,
verse8
siku nyingi nimesikia makelele
kwa wanandoa ,
lakini chanzo ,ni wewe mama mkwe,
lakini taabu ni wewe mama mkwe,
nasema tafrani,ni wewe mama mkwe,
kuvunjika ndoa za watoto wenu
tatizo ni mama mkwe,
mama jirekebishe mama mkwe,
nasema jirekebishe unatia aibu,
message sent ukidelete ujumbe
umefika,
(aibu we )x3
unatia aibu x6
No comments:
Post a Comment