Tuesday, May 3, 2016

AKUTENDEE NINI LYRICS BY CHRISTINA SHUSHO


 halleluyah,yesu ni bwana na wala hana mpinzani

Wataka akutendee nini,akutendee nini wee,x2

(neno moja nalitaka kwa bwana,nalo ni hili,
nikae nyumbani mwake,siku sote za maisha yangu)
ghala lake limejaa hakuna aliyepunguza ata robo,
akutendee nini wee,

wengine wanataka kuwa rais wa nchi,
wengine wataka ubunge ,nawe akutendee nini wee,
wengine ombi lake apate shamba,huyu mume na huyu mke
wataka akutendee nini wee

mama huyu ombi lake apate mtoto,mwingine apate elimu,
wataka akutendee nini wee,(mwambie x2 eh)

Wataka akutendee nini,akutendee nini wee,x2

nakumbuka mgonjwa birikani,miaka thelathini na nane,
alikuwa hajiwezi yeye,yesu katembelea birika vile,
akamwona mgonjwa yule mara akaanza sababu zake,
malaika akifika anaingia kisimani,anatimua maji,
na mimi nakuwa wa mwisho,wataka akutendee nini wee,
yesu akasema neno moja jitike gondoro lako na uende,
mara akawa mzima eh

Wataka akutendee nini,akutendee nini wee,x6No comments: