Wednesday, December 14, 2016

AMINI LYRICS BY GLORIA MULIRO

Verse 1:
Tangu niwe mdogo,
ni mengi nimepita
Mengine mazuri,
mengine machungu
Lakini jambo moja aaa ninalijuwa
Heri mwisho wa jambo, kuliko mwanzo wake eee, oooo! x2

Chorus:
Amini mwenzangu (Mungu atakuweka juu)
Amini moyoni (Mungu atakuweka juu)
Usiwe na shaka (Mungu atakuweka juu)
Usiwe na hofu (Mungu atakuweka juu)
Hata kama uko chini (Mungu atakuweka juu)
Hata kama umeshindwa (Mungu atakuweka juu)
Usiwe na shaka (Mungu atakuweka juu)
Usiwe haraka (Mungu atakuweka juu)

Verse 2:
Mwanzo nilivyokuwa, mimi sikuchagua aaa
Yote niliyopitia, mimi sikuchagua aaa
Kukosa chakula, mavazi, amani sikuchagua
Kudharauliwa, kuteseka, kupotea njia sikuchagua aaaa
Ila Nashukuru Mungu alitumia yote kunitengeneza aaaa, eeee!!

(Chorus)

Verse 3:
Mwanzo wako najua haukuchagua
Japo mambo uliyopita wewe hukuchagua
Lakini amini hayo Mungu anakwambia
Macho hayajaona masikio hayajasikia
Mambo makubwa amekupangia

Chorus :

No comments: