Tuesday, July 7, 2015

TENDA WEMA LYRICS BY ROSE MUHANDO

Woi Woi Woi eh, Nenda
Tenda wema nenda zako, nenda,
Usingoje Kusifiwa, mama we,
Usisubiri ahsante, nenda,
usingoje shukurani mama we, nenda
Wanadamu si wema, mama we
Wana meno wanauma, mama we,
Wanawasha kama pilipili, mama we,
Wana ukupu utajikuna we, mama
Meno yao kama chuma, Mama,
Tenda wema nenda zako utalipwa na mungu,

Ukisubiri kusifiwa, Mama we,
Ukingoja shukurani we, mama we,
Makubwa yatakukuta, Mwenzangu we,
Makubwa yatakukuta, pole we,
Matusi utayasikia, Pole we,
Dhihaka utazitambua, mama we,
Kashifa utatupiwa,mama we,
Tenda wema nenda, zako, mama
Nasema usigeuka nyuma, Nenda X2
Nasema nenda, utalipwa na mungu.


Siku ya mateso yako, pole we,
Siku ya mateso yako mama, pole we,
Siku ya huzuni yako, mama,
Siku ya mahangaiko yako,
Siku ya anguko lako, mama, pole we,
Waliokuwa rafiki zako, baba,  watageuka  mwiba kwako, pole
Waliokula chakula chako , mama, watageuka anguko lako,
Uliotenda wema kwao, pole we,
Yatageuka maumivu yako,pole we
Waliokula chakula chako, siku ile,
watasahau wema wako, mwenzangu we,
Watakaa vibarazani,  jamani eh,
Watacheka na vicheko, mama we,
Majina watakupatia, pole we,
Tena mabaya yenye hatia, tena,
Tena mabaya yenye udhia, kwako,
watakwita kimbelembele, kimbelembele
eti wewe kimbelembele, mwenzangu kimbelembele
wema wako kimbelembele, kimbelembele
uliwasaidia kimbelembele, kimbelembele X2
Mama , mama we X3
usichoke kutenda wema, utalipwa na mungu

Wacha niseme ukweli, jamani eh,
Wacha niseme ukweli, mwenzangu eh, 
wanadamu hawabebeki, hawabebeki
ata ukifanya nini, Hawabebeki,
Wabebe kwa mbeleko ya chuma, hawabebeki,
wabebe kwa maturubai, hawabebeki,
watachukua na viwembe jama eh, mama
watachana turubai, kweli, wachane wakukimbie,
Wabebe kwa mbeleko ya chuma, hawabebeki,
watatafuta misumari jama, mama,
wagonga ngo! ngo ngo X3
Wape chakula wale, haiya,
washibe wakutukane jama, mama
Wape chakula wale, tena, kesho watakushitaki,
nenda, nenda , ah nenda, utalipwa na mungu.




3 comments:

4llowed said...

Nice blog. Thank you for the lyrics.Be blessed. Please post "Tabu Zangu"

Lexo22 said...

Thank you so much for this wonderful lyrics. I so much love this song even though I don't understand the meaning.

Anonymous said...

Could be good to let us copy the text to be put in a translator, that way will let us understand what is the lirycs saying.