Tuesday, April 4, 2017

UNIKUMBUSHE LYRICS BY BAHATI AND RAYVANNY


(Usiponiona leo kama jana kesho nikumbushe
nisipokuwa leo kama jana kesho unikumbushe)x2
(nikumbushe eh
unikumbushe eh) x2


Leo nyota imeng'aa
nasahau nilikotoka
naidharau mitaa
na mateso niliyosota, aie
ndugu zangu kinyaa
mafukara wananichosha
niache wafe na njaa
nijisifu nitawanyosha eh


sili kwetu Kisumu bondo,
chakula haina swaga,
sitaki kula chapo dondo
nataka pizza na buger ehh,

uniepushe maulana nisiishie njiani,
unikumbushe ya jana, kesho nipe dhamani
kwenye maisha ya muziki, ukiwa na uendo utaishi
Timu hazijengi urafiki, tusije kuuana kwa kugombania viti
eti nimuache mama kwenye dhiki, kisa mambo yangu yametiki
akipiga simu siishiki, nikipokea nimwone kama shabiki

(Usiponiona leo kama jana kesho nikumbushe
nisipokuwa leo kama jana kesho unikumbushe)x2
(nikumbushe eh
unikumbushe eh) x2

nimejawa na kiburi, ukweli haupo nami,
alionifunzage dini mama, simwiti mummy,
roho imejawa na uhuni, star najiona mi
nikipita na kagari vumbi , natupia wadhee
niwe kama peter, kumkana yesu mara tatu nikumbushe
niwe kama jonah, kukataa kutumwa nineveh nikumbushe
ah mwanabujah alionipa suporti, namtusi ilimradi iwe kiki
walionipa jina mashabiki leo, nawaona wanafiki

(Usiponiona leo kama jana kesho nikumbushe
nisipokuwa leo kama jana kesho unikumbushe)x2
(nikumbushe eh
unikumbushe eh) x2

1 comment:

Unknown said...

Unikumbushe ya jana, kesho nipe thamani
Kwenye maisha ya muziki, ukiwa na upendo utaishi