Sauti ilisikika mjini ramah,
Kilio na maombolezo mengi,
Reali akiwalilia watoto wake,
Lakini hakutaka kufarijiwa kwa kuwa hawapo tena
Bwana asema hebu zuia sauti yako, usilie mama,
Na macho yako, yasitoke machozi , tulia eeh jipe moyo.
Maana kazi yako itapata dhawabu,
Na kwa nguvu mpya, nguvu mpya utainuliwa tena,
Wakati tulio nao, si wa kuomboleza tena,
Siku za kilio zimepita zimekwisha , aha
Sasa twasonga tena, mbele kwa kazi yake bwana,
Matukio kamwe hayatatukatisha tamaa ,
Na tutaweza yote,kwa jina lake mwenye nguvu,
Na kwa mkono wake yeye mwenyewe atatuongoza
Twatiwa nguvu kwa neno lake bwana mungu,
Asemapo baada ya hayo yote nitarejea,
Nami nitaijenga tena nyumba yake daudi ,iliyoanguka,
Nitajenga tena maanguko yake , nitaisimamisha,
Kwa ajili yake bwana twaweza kuuwawa mchana , usiku kucha,
Twahesabiwa kuwa kama kondoo wasubirio kuchinjwa,
Lakini katika mambo hayo yote tumeshinda na zaidi ya kushinda kwa yeye aliyetupenda jina lake lisifiwe milele,
Baada ya siku hizo za kupigwa vikali,
Kama alivyoahidi nguvu mpya, ametupatia tena
Wakati tulio nao, si wa kuomboleza tena,
Siku za kilio zimepita zimekwisha , aha
Sasa twasonga tena, mbele kwa kazi yake bwana,
Matukio kamwe hayatatukatisha tamaa ,
Na tutaweza yote,kwa jina lake mwenye nguvu,
Na kwa mkono wake yeye mwenyewe atatuongoza x3