Thursday, May 7, 2015

NALILIA UZIMA LYRICS BY AIC SHINYANGA CHOIR

Nalilia uzima, kutoka kwa Bwana
Ili nikaishi naye katika uzima,
Uzima wa milele
Shetani anaulilia uzima wangu mimi,
Anisukumia mawimbi ya kila haina
Na mateso makali X2


Anitisha ili nisimuone Bwana
Lakini nimejitoa ,  Kwa bwana kwa moyo wangu wote
Liwalo na liwe
Asukuma silaha za maangamizi, eti anisambaze,
bwana wangu kaniwekea walinzi,
Najivuna kwa bwana.  X2

Shetani hana nafasi,
kwangu mimi moyoni mwangu
yesu atawala , uzima wangu, niliopewa na bwana X2

Uzima wangu ni wa dhamani,
gharama yake kifo chake yesu,
dhamani yake ni damu yake,
bwana yesu msalabani. X2

Yesu ni nuru  moyoni mwangu,
yesu ni uzima wangu,
yesu ni ushindi , namtegemea yeye katika kila jambo,
siogopi kitu , bwana ni ngome yangu,
sibabaishwi kitu. X2

Nalilia uzima, kutoka kwa Bwana
Ili nikaishi naye katika uzima,
Uzima wa milele
Shetani anaulilia uzima wangu mimi,
Anisukumia mawimbi ya kila haina
Na mateso makali X2

yesu, u-natosha, u-natosha, wewe peke yako
shetani, u-shindwe, u-shindwe, kwa jina la yesu  X2


Anitisha ili nisimuone Bwana
Lakini nimejitoa ,  Kwa bwana kwa moyo wangu wote
Liwalo na liwe
Asukuma silaha za maangamizi, eti anisambaze,
bwana wangu kaniwekea walinzi,
Najivuna kwa bwana.  X2








No comments: