Tuesday, August 30, 2016

HATUA MOJA LYRICS BY WILBERFORCE MUSYOKA

(Nataka hatua moja zaidi, oh Baba hatua moja zaidi)

Chorus
Ninachotaka kutoka kwako, ni hatua moja zaidi x2
Eh Yesu uu zaidi na zaidi x2


verse 1
Neno lako ndilo nuru na taa ya miguu yangu x2
Kutoka hatua kwenda hatua, Baba nimulikie x2
Ooh Baba nimulikie,
ninachotaka kutoka kwako, hatua moja zaidi
(Mulika Baba, Mulika Yesu) x2

(Chorus)

verse 2
Nimekaa nilipo kipindi cha mapito kwa muda mrefu x2
Marafiki zangu wamejenga manyumba, nimebaki
Marafiki zangu wamenunua magari, nimebaki
(Wengine wamesomesha, Mimi tu nimebaki) x2
Oh Baba nipe hatua moja, Oh Baba hatua moja zaidi

(Chorus)

verse 3
(Nimejaribu kila njia, hakuna linalosonga) x2
Hekima talanta hakuna linalosonga
Elimu hakuna linalosonga
Sasa macho yangu, Baba yako kwako,
leo macho yangu, Baba yako kwako,
Nipe tu, hatua moja zaidi,
Baba nipe, hatua moja zaidi

(Chorus)

verse 4
Zaidi na zaidi tunasonga mbele
(Nawe) x4 Yesu, tunasonga mbele
Katika safari yangu, ni wewe nakuhitaji Baba
(Nawe) x4 Yesu ninasonga mbele
Katika nyumba yangu, na biashara yangu Baba
(Nawe) x4 Yesu ninasonga mbele
Wewe na Mimi Baba, Mimi na wewe Yesu
(Nawe) x4 Yesu ninasonga mbele
Nipe hatua moja zaidi Baba nisonge na wewe mbele
(Nawe) x4 Yesu ninasonga mbele

No comments: